Ni miaka arobaini na tisa ya maazimisho ya muungano wa yaliyokuwa mataifa mawili huru kutoka mikononi wa uangalizi wa wakoloni kwa niaba ya umoja wa mataifa yakijulikana kama TANGANYIKA na upande mwingine VISIWA VYA ZANZIBAR. ..kihistoria ni mataifa mengi sana yalifuata njia hizi za kimuungano katika kuweka tija kisiasa,kiuchumi na hata kiutamaduni ikumbukwe umoja wa nchi za kisosholisti(USSR) ,west Germain and east Germain(GERMANY) ,GREAT BRITAIN na mifano mingi lakini Muungano kati ya TANGANYIKA na ZANZIBAR ni tunu inayoendelea kuishi ikiwa hai kwa kipindi kirefu.TANZANIA ni mfano wa kuigwa sana katika dunia inayoamini umoja katika kuleta tija kijamii katika nyanja zote...ni kweli kabisa muungano wetu ni wa kimakubaliano kati ya viongozi wetu nguli na inawezekano haukuwa na tija ya kimkataba(ÀGREEMENT ACT) na ulikuwa umeshamili katika (Memorandum of understanding) na baada kuingizwa katika 1977 CONSTITUTION OF TANZANIA kama alama kuu ya kuubaliki muungano.Kwa tafsiri hiyo wengi wamekuwa wakiubeza muungano huu ila ni makosa kusema hakukuwa na muungano kwani muungano upo na upo hai kwa watanzania wa bara na visiwani. ..kuna mengi ya kujivunia kwa kipindi chote na tunaitaji kutambua muungano ni nuru inayoitaji a continuity of Agreement Act kwa mantiki hiyo uwepo wa uundwaji na utengenezaji wa katika mpya ni tunu nzuri wa kuujadili kwa nia ya kuuboresha na kutumia fursa hii kuuwekea misingi imara na kuondoa kama si kumaliza kasoro za kimuungano. ..napenda kutumia fursa hii kama mtanzania mzalendo kupongeza watanzania wote kwa kuwa na mshikamano na kudumisha amani kwa kuwa na mioyo ya kiutu na uvumilivu uliotukuka pamoja na changamoto zake..maamuzi yetu ya busara na hekima ni neema itakayo tukuzwa sana na vizazi vijavyo..mungu ibariki tanzania mungu ubariki muungano wetu
No comments:
Post a Comment