Ni miaka arobaini na tisa ya maazimisho ya muungano wa yaliyokuwa mataifa mawili huru kutoka mikononi wa uangalizi wa wakoloni kwa niaba ya umoja wa mataifa yakijulikana kama TANGANYIKA na upande mwingine VISIWA VYA ZANZIBAR. ..kihistoria ni mataifa mengi sana yalifuata njia hizi za kimuungano katika kuweka tija kisiasa,kiuchumi na hata kiutamaduni ikumbukwe umoja wa nchi za kisosholisti(USSR) ,west Germain and east Germain(GERMANY) ,GREAT BRITAIN na mifano mingi lakini Muungano kati ya TANGANYIKA na ZANZIBAR ni tunu inayoendelea kuishi ikiwa hai kwa kipindi kirefu.TANZANIA ni mfano wa kuigwa sana katika dunia inayoamini umoja katika kuleta tija kijamii katika nyanja zote...ni kweli kabisa muungano wetu ni wa kimakubaliano kati ya viongozi wetu nguli na inawezekano haukuwa na tija ya kimkataba(ÀGREEMENT ACT) na ulikuwa umeshamili katika (Memorandum of understanding) na baada kuingizwa katika 1977 CONSTITUTION OF TANZANIA kama alama kuu ya kuubaliki muungano.Kwa tafsiri hiyo wengi wamekuwa wakiubeza muungano huu ila ni makosa kusema hakukuwa na muungano kwani muungano upo na upo hai kwa watanzania wa bara na visiwani. ..kuna mengi ya kujivunia kwa kipindi chote na tunaitaji kutambua muungano ni nuru inayoitaji a continuity of Agreement Act kwa mantiki hiyo uwepo wa uundwaji na utengenezaji wa katika mpya ni tunu nzuri wa kuujadili kwa nia ya kuuboresha na kutumia fursa hii kuuwekea misingi imara na kuondoa kama si kumaliza kasoro za kimuungano. ..napenda kutumia fursa hii kama mtanzania mzalendo kupongeza watanzania wote kwa kuwa na mshikamano na kudumisha amani kwa kuwa na mioyo ya kiutu na uvumilivu uliotukuka pamoja na changamoto zake..maamuzi yetu ya busara na hekima ni neema itakayo tukuzwa sana na vizazi vijavyo..mungu ibariki tanzania mungu ubariki muungano wetu
thank you as a friend,relative and close friend to me because your reason to this success
Friday, April 26, 2013
Friday, April 12, 2013
Mtazamo wangu katika mdahalo wa leo juu trh 12 februari 2013 azimio wa Arusha vs Dira ya Maendeleo 2025
Awali ya yote ningependa kukili wazi kuwa katika jamii ya watu wengi walio na kipato cha chini ,wanaoishi low of per capital income of one dollar zaidi ya asilimia 76.5, mfumo angalau utakao wakomboa katika uzalishaji mali kuwa ni Ujamaa(socialist ideology) kwani misingi ya azimio la arusha 1967 kwa imani yangu mimi lilizaliwa katika mfumo wa kijamaa ndo maana misingi ya USAWA,UTU na miiko ya kiuongozi ilizingatia mfumo wake wa uzalilishaji mali kwa kwa mfiringo huo tunapata tafsiri ya Azimio la Arusha kuwa ni "chapisho la kimsingi lilikuwa na lengo la kujenga jamii inayoeshimu misingi ya utu na usawa katika kumiliki uchumi na kugawanya raslimali za nchi". ..ni wazi kuwa hata kabla ya azimio kuanzishwa 1967 sababishwa hasa ilikuwa ni first tanzania vision after political independence ikiwemo matabaka ya wanaotaka kumiliki uchumi ambao enzi hizo waliitwa kUPE(leo Mafisadi) azimio lilibainisha wazi mbinu na malengo ya kuwaua hao kupe...kwa kujenga jamii ya kijamaa, zambi ya fitina na unafiki kama ilivyotafsiriwa na mwalimu katika machapisho yake ni wazi kuwa ulizungukwa na watu walio na imani tofauti tofauti za kiitikadi na kiimani ambao kwao ubinafsi ulikuwa sehemu kubwa katika maisha yao bila kujali mass situation and intetests...1980's ni kipindi kigumu zaidi baada ya nchi kujishughulisha katika vita vya kagera kama effects mojawapo ya kudondoka kwa mfumo wa miimili ya vita ya kidora ya kikomunisti na kipepari (bi-polar system ) na kubaki na mfumo wa single powerful system(ubepari) kwa bahati mbaya sana kutokana na athari za vita na baa la njaa 1980's, Taifa lililadhimika kukubali mfumo usiopendwa kuabudiwa na walio madarakani kwa kuutamka kwa umma, mfumo wa kinyonyaji, unapandikiza misingi ya kibinafsi na umimi kwa kulipokea na kuliabudu mpango wa maendeleo ulioitwa STRUCTURAL ADJACEMENT PROGRAMME(SAP) ambao ndio uliobadili kabisa misingi ya mwalimu wa kupandikiza Imani mpya kwa vizazi vya 1980's, 1990's,2000's ambao hawa wamelelewa na kukuzwa katika misingi ya kimfumo huu....utu na usawa ikiwa vita ya kifikra kwa wapenda maendeleo ya wengi. Na rushwa,mifumo ya kinyonyaji ikaanza kushika hatamu kwa kasi sana na ndipo tunapanda dhana mpya ya DIRA 2025. ..napenda nieleweka sina kasoro na dira hata kidogo kwa maana kwamba ni imani yetu kuwa lengo lake ni kuamsha kasi ya maendeleo ya watanzania lakin ikumbukwe basic yake ni katika mfumo upi?misingi yake ilijikit katika misingi ya kipepari ambapo ndio ilishamili kwa sasa. .kwa ufupi sana DIrA sio jibu kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na wakulima wachini ambao ni asilimia 75% ya watanzania labda tusaidiane tafsiri hapa ni wazi kuwa kutazalishwa kwa tabaka la watu wa juu wachache wamiliki uchumi, tabaka la kati la watu wnaomiliki uchumi wa kati na wengi wa watabaki kuwa tabaka la chini ambao lengo kuu la azimio lilikuwa kuondoka kama sio kuua mifumo hii ya kimatabaka.
NI NINI TUFANYE KWA SASA?
1-Tutambue wazi mfumo pekee wa uzalishaji mali ambao Mwalimu aliuona si kwa kuwa kina Mao Tse Tung wa china alikuwa rafiki tu ila ndio jibu la kiukombozi la Masikini tukitumia china model ni mfumo wa kijamaa ambapo utajenga ufumo wa kujitegemea kisiasa na kiuchumi
2-Misingi ya azimio la Arusha ni lazima itukuzwe na kuingizwa katika katiba mpya, ANGALIZO Ni lazima tukubali kurudisha jamii ya kikomunisti ili tuweze kuitekeleza misingi hiyo la sivyo tusiote katika hilo
3-kama taifa tuwe tayari kujifunga mkanda kwa kipindi kisicho pungua miaka 10 cha mpito kwa tafsiri kuntu cha maumivu ya kuchuma kabla ya kujenga jamii toka utegemezi na yenye kujitegemea yenyewe
4-kipindi hicho chote kuheshimiana,kuvumiliana na kupendana kama wamoja ndio jibu la mafanikio
Kwa mantiki hii, azimio la Arusha ni muhimili wa ukombozi na naungana na Dr.Willy Mtunga(jaji mkuu wa kenya) katika kusambaza virusi vya azimio la Arusha kwa maana ya kuelimisha watu na kutoa tafakuri anuwai juu ya maana yake na umuhimu wake kwa jamii ya watu masikini
Wednesday, April 10, 2013
Prof mkandawire biography
Professor Thandika Mkandawire - Who's who - International Development - Home
Prof thandika mkandawire openly the fifth julius nyerere intellectual lecture "reflections on pan africanism and alternative paths to development" the main works and biography of Prof Mkandawire