Leo katika wazo kuu hapa tunaangazia na kujaribu kufikirisha na kujifikirisha juu ya mkutano utakaofanyika alhamisi hii ya februari 13 2014 kule uingereza chini ya prince of wales,duke of cambridge ,David Cameroon and William Hague ,Rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania ,Mh Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kati yaya viongozi 50 watakao wakilisha nchi zao katika mkutano huo ,huku kukiwa na majadiliano makali yakiendelea juu ya ripoti ya ujangili wa tembo nchini Tanzania na ikikumbukwa kuwa agenda muhimu ya mkutano huu ni juu ya kufikia mikakati ya ulinzi wa viumbe hai na imadhamiriwa kutumika zaidi ya euro 5 billion kupambana na ukatili huo wa viumbe hai ,sio jambo jipya sana hapa kwetu kwani uliibuka mjadala uliopelekea kujiuzulu kwa baadhi ya mawaziri juu ya ripoti ya mapambano ya ujangili ikijulikana kama operesheni tokemeza ujangili ambayo utekelezaji wake ulikithiri katika vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kutajwa kwa watu wengi hasa viongozi waandamizi wa serikali na watu maarufu nchini na wakihusishwa kufanya biashara hii na wanaoitwa ni wafadhili na marafiki zetu katika maendeleo...Katika taarifa ya makala moja katika gazeti la MAIL la uingereza limejaribu kuhusisha hili na mahusiano yetu kimataifa hususani na bara la asia kama watekelezaji wa biasharra hii haramu na nchi baadhi za Afrika (.http://www.dailymail.co.uk/news/article-2554773/Tanzania-slaughters-11-000-elephants-year-bloody-trade-tusks-President-turns-blind-eye-Prince-really-shake-hands-him.html)
1-tuzitafakari na kuzijadili kwa kujihadhari na hizi dalili nazoziita mvutano wa kimaslahi katika jumuiya ya kimataifa ,China na Tanzania ni marafiki wa kihistoria na hata kwa kipindi kirefu walikuwa wakiamini katika itikadi na kujenga mising ya kimaendeleo katika falsafa zilizokuwa zikifanana ,hofu yangu katika hili ni tunaweza kukubali kutumika katika kuaminishwa katika yale ambayo hayatakuwa sahihi sana ,hatutaweza kugharamikia gharama za chuki na fitna za watu ambao tunamfanano mzuri wa kihistoria na hata kiitikadi ,tunaitaji kuwa makini sana katika hili.
2-tuheshimu sana masslahi yetu kwa nguvu na mali ili kujilindia heshima yetu kitaifa na hata kimataifa kwa kuamini kuwa maslahi yetu hayatakuja kuaminishwa kuwa na mashirikiano na taifa lolote lile ila hatasita kuhusiana na yeyote yule atakayekuja kwetu kama rafiki na atakaye heshimu sera zetu za nje na atakaye heshimu maslahi yetu katika uhusiano huo.
3-Tatu na mwisho tuamini kuwa taifa letu ni changa na ni taifa huru mshikamano wa "kulinda maslahi na kutetea maslahi yetu utaongozwa kwa fikra zetu na maamuzi yetu kwa maridhiano yetu kwanza" na ushauri na maamuzi ya wengine yatafuata minyororo ile ile ya fikra zetu na maamuzi yetu kwa lengo kuu la kimsingi kuboresha na kamwe sio kuondoa maslahi yetu kwa kukithi tija na nia ya maslahi ya wengine kwa rasilimali zetu za ndani ya mipaka yetu.
Katika huru wa mwanadamu moja ya nyenzo kuu ninayoiamini ni uhuru wa fikra katika kutafakari na kutafakuri juu ya hoja..hivyovtuendelee kufikiri na kujadili juu ya hayo ili kujenga wazo kuu....
...........Asanteni kwa kuwa nami sasa tujadili tena katika wakati mwingine........
thank you as a friend,relative and close friend to me because your reason to this success
Monday, February 10, 2014
Sunday, February 9, 2014
umuhimu na tija ya kuhimizana kama vijana juu ya kusomana kuwekeza katika elimu lecture
PRESENTATION
Comrade
Yusuph KAMOTE
INSPIRATION FOR YOUTH STUDENTS PROGRAM
GHOMME
SECONDARY SCHOOL 08/01/2014
Awali ya
yote napenda kutumia fursa hii hadhimu kumshukuru mwenyezi mungu ,muumba mbingu
na ardhi kwa kutupa wasaha mzuri wa kunikutanisha mimi pamoja nanyi vijana
wenzangu mchana huu.
Katika hali
ya unyenyekevu mkubwa nimesimama mbele yenu si kama kiumbe mbora kuliko ninyi
vijana wenzangu ila kama kijana mtiifu na mtumwa wa fikra za kuamini katika
kukumbusha ,kuhamasisha na kujifunza kutoka kwenu juu ya masuala mbalimbali
yenye athari chanya katika jamii zetu,hususani leo tunapozungumzia juu ya elimu
na umuhimu wake kwa nafsi zetu na kwa taifa letu.
Elimu kwa
mara kadhaa tumesikia ikiwa na kila maana ya tafsiri inayojaribu kutoa maana
kuwa ni ujenzi wa kujikomboa ,kujiongoza na hata muhimili muhimu wa kupambana
na changamoto mbalimbali katika jamii tunazoishi ,katika ujenzi wa taifa changa
kama taifa letu Tanzania elimu ni msingi wa kutoa unyonge ,uonevu na
ukandamizwaji wa minyororo ya umasikini wetu, hivyo kupitia siku hii
nitawaomba kwa pamoja tutangaze vita ya kujikomboa,kujinasua na kujenga fikra
pevu kupitia kusoma,kujifunza si kwa maana ya kuchukua fikra za kale kama
silivyo na kuishi nazo leo hapana ila ni katika kujenga fikra mpya katika
kukabiliana na changamoto za leo ili kuleta tija ya maendeleo na kasi ya
maendeleo ya kidunia ,kama taifa tunaitaji sana wahandisi wengi,madaktari wengi
katika fani tofauti tofauti ,tunaitaji wanasheria wengi ,tunaitaji wataalamu
waliobobea wa masuala ya kitawala na kisiasa,tunaitaji sana sana wasomi wengi wa
masuala ya utawala wa biashara na wahasibu na fani mbalimbali ,
SWALI LINAKUJA TUNAWAPATA VIPI NA WALIOJENGWA KWA FALSAFA
ipi ya kielimu?
Katika
kulijibu swali hili nitajielekeza katika sehemu mbinu kwanza kutoa moja ya
dhaifu lililopo katika mfumo mzima wa elimu yetu na kutoa njia za kunasuka huko
na kisha nitasema tutafika vipi huko ,naitaji usikivu wenu ulio tukuka hapa ;-
DHAIFU KUU-Moja ya dhaifu kubwa sana
ninalofikiri mimi ni mfumo wa elimu yetu kukosa falsafa ya kuwajenga watu
waamini katika nini na wanapaswa kuwa na majukumu gani kwa taifa lao ambacho hiki kingelijenga tija
ya wasomi wetu kujielekeza na kujiaminisha kuwa wao wanajukumu la kiukombozi
katika taifa lao.
Madhara ya
kuwa na mfumo usiojengeka katika falsafa yeyote ni watu kuamini katika yale
yanayowaathiri katika jamii badala ya wao kuwa wahusika katika kutoa athari kwa
msimamo wa kimfumo uliowalea(falsafa ya kielimu)
Mawazo yetu vijana
wengi kuwa tunasoma ili kupata vyeo vikubwa(manager,officer,director,mbunge,waziri,rais)
na kisha kuwa matajiri kwa kujihifadhia pesa nyingi kulikotokana na kusoma
kwetu hii ni athari ya kijamii inavyoamini kwa mtu msomi, Ila mimi naomba
kuiita hii ni athari ya Kukopa utamduni na kukosekana kwa falsafa ya elimu yetu
kama taifa.
Kwa pamoja
tuamini maisha ni hatua na hatua hizo huitajika sana mipango ,ufahamu na
uelewa/weledi wa kupambana na changamoto zake na pesa,vyeo na mafanikio ni matokeo ya vitu vinne ambavyo leo nitavitumia kama jinsi gani tunaweza pata
mafanikio katika kusoma kwetu na hata katika maisha yetu
JUHUDI/BIDII
Nafahamu kuwa msamiati huu katika mazingira haya ni msamiati
wa kawaida sana ,ninaamini walimu na hata miongoni mwenu inawezekana kuwa na
utamaduni wa kukumbushana juu ya kuongeza juhudi na bidii katika masomo yenu
,hivyo sitatumia mda mwingi sana hapa ,ila nachopenda kuwasihi vijana wenzangu
juhudi pekee ndio siri ya mafanikio katika masomo yetu na hapa mahali popote
pale panapoitaji ufanisi lazima juhudi iwepo ili tufikie mafanikio tunayojiwekea.
MAARIFA
Maarifa ni dhana pana ila ni kati ya yale tunayojifunza na
kuyasoma kwa kujenga mazingira ya kujifunza zaidi ya yale walimu au mkufunzi
anayotupa darasani kwani ,tunayapata vipi haya maarifa ni kupitia kupenda
kusoma vitabu vya ziada juu ya mada tunazojifunza kwa lengo la kupanua zaidi
uelewa wetu na kuyatumia hayo maarifa vyema zaidi katika mitihani na hatac
maisha yetu na hapa ni vyema tujiwekee mazoea ya kupenda kusoma vitabu sana
.
MAADILI NA NIDHAMU
Kwa upande wangu ninaamini hiki ni kiini cha mafanikio
masomoni na hata maishani ,kwani kwanza kitakujengea heshima na upendo kwa
walimu na hata kwa jamii inayokuzunguka na watu watapenda kushirikiana nawe
katika shughuli zako za kimasomo(discussion group),nina imani hapa shuleni kuna
idara maalum na mwalimu wa nidhamu ambae kwenu kwa wachache wenu umuona kama
adui ,mnoko wao lakini nataka kuwa shuhuda wenu leo huyu ni kiumbe bora kwenu
kwani anasimama katika mafanikio yenu ya baadae,anawezaje na unaweza kumtumia
vipi huyu?nina amini shule na hata nyinyi wenyewe mna timetable zenu ,moja za
sifa za wengi waliofanikiwa ni wanaoheshimu na wenye nidhamu juu ya muda wao na
mipango yao,nanyi mtakuwa kati ya waliofanikiwa kama mtaheshimu muda na mtakuwa
na nidhamu juu ya utumijai wa muda wenu nyakati hizi za masomo yenu.
USHIRIKIANO NA WIVU WA KUFIKIA MALENGO
Nakumbuka kwa ukaribu mkubwa mara Zote nimekuwa nikiamini
kuwa “kila binadamu mbele yangu ni faida na nimesogezewa kwa lengo
moja tu kufaidika kwa uwepo wake” hii
ikiwa na nana kuwa binadamu sisi tumebeba mema na mabaya katika tabia na
mienendo yetu ,jukumu letu ni kujifunza vyote ili kuweza kujinasua na kuyaepuka
yale mabaya yatakayo athiri malengo yetu na kushikamana na yale mazuri yatakayo
boresha ukaribu wa kufikia mafanikio yetu
,hivyo basi kujengea ushirikiano wa kila mmoja wetu katika masomo
itatuwezesha kwa pamoja kufikia malengo katika masom yetu.
Kingine kama ziada ambacho ni cha msingi mno ni
kuwashughulisha walimu kama sehemu ya kuwatumia katika kufikia malengo yako ya
kujizidishia maarifa zaidi na kuhakikisha unamtumia yeye kama chombo chako cha
kufikia ufaulu mzuri .
Kwa ujumla ukijiwekea misingi hii yote kama sehemu yako
katika masomo na hata kimaisha jua utazalisha kile kinachokiita mafanikio
katika maisha yake ni hizo pesa zitakuwa matokeo ya misingi ya hivyo vyote
nilivyokwsisha waeleza vijana wenzangu.
Kwa kumalizia niwasihi tena na tena kuzingatia niliyowaeleza
na watoa hoja wenzangu katika mhadhara huu waliyokwisha na watakayowaeleza .
Kwa mara nyingine tena niwashukuru sana tena sana Africa
Youths Leadership Mark (AYLM TANZANIA) kwa mawazo na nia yao ya kudhubutu
kuwafikia vijana na kuongea nao katika yale yenye tija na maslahi kwa taifa
letu na pia niwashukuru kwa mualiko wao wa kunialika nije nitoe lecture hii
kwenu kama kijana mwenzenu ,nawashukuru
sana.
Mwenyezi
mungu awape wepesi katika masomo yenu na awajalie nyie pamoja na taifa letu
katika vita hii niliyoitangaza leo ya kujikomboa kupitia elimu ,sasa tupo
mapambanoni na tusichoke kupigana paka mwisho .
ASANTENI
SANA KWA KUNISIKILIZA
Subscribe to:
Posts (Atom)