Leo trh 08 Mwezi disemba ilikuwa kuhusu Rasilimali zilizopo nchini na nafasi ya Mtanzania juu ya Rasilimali za nchini kwake....... .
Kimsingi kwa nadharia na mtazamo wangu, mimi naamin pamoja na mambo mengine yaliyozungumziwa nijikite katika mambo makuu mawili nayo ni yafuatayo -:
-KUAMINIANA na
-USHILIKISHWAJI WA MWANANCHI NA RASILIMALI ZAKE
KUAMINIANA
Hii ni dhana ya msingi katika jamii yenye malengo na mikakati katika maswala yanayowahusu .
Nitoe mfano mmoja katika kuonesha faida zinazopatikana hasa kwa kiongozi kujenga imani ya kuwaamini anaowaongoza ambao kimsingi ndio wamiliki wa kwanza wa ardhi na wadau wakuu wa maendeleo kwani yanawahusu moja kwa moja wao..Moja ya matajiri wakubwa katika bara la Afrika ni Dangote lakini niliwahi kupata kusikia historia yake ya kutoka kuwa cement importer to cement processing and manufacturing na imemjengea uwezo mkubwa kiuchumi na hasa kuchangia 3.5 billion USD kwa pato la mwaka katika nchi yake ,lakini haikuwa rahisi kwa dangote kupata mafanikio hayo peke yake ila iliwezekana kwa ushauri na kuaminiwa kwake na moja ya viongozi na serikali yake ndio imekuwa sababu ya utajiri wake ambao ni nuru kwa maisha ya Wanigeria leo hii.
Pamoja na ukweli kuwa uwezo wetu katika uchimbaji, umilikaji na uzalishaji wa nishati mbalimbali ikiwamo gesi ni mdogo na uenda ikawa ni vigumu kwetu lakini haiondoi ukweli kuwa bado mali hii ni ya Watanzania na hivyo wanastaili kufaidika moja kwa moja kupitia rasilimali zao na hata ikiwezekana wao kuwezesha na kuaminiwa kama walivyotengenezwa kina Dangote .
Katika hoja ya ushilikishwaji naomba niishauri serikali na Watanzania wenzangu kuwa "serikali na wadau wa maendeleo kuelekeza kupitia sheria mama/rasimu ya katiba mpya isomeke kuwa waratibu wakuu na mwenye maamuzi ya mwisho juu ya nani amiliki rasilimali fulani ndani ya maeneo ya wazawa wawe wanakijiji mwenyewe" kupitia maamuzi ya pamoja katika muundo wa "mkutano mkuu wa kijiji "kwani ushilikishwaji wao kwa sasa unaonesha madhaifu makubwa ,kwa ukweli kuwa umekuwa wa kinadharia sana kuliko uhalisia hivyo :
Tubadili dhana kuwa vyombo vya dola au halmashauri kuwa waamuzi wa mwisho bali wabaki kuwa wasimamizi na watekelezaji sera katika maeneo husika ila wasemaji wa mwisho juu ya rasilimali zao wawe wazawa/wanakijiji/wananchi hii itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi ikichochewa kwa kiasi kikubwa na Rasilimali zilizopo katika ardhi husika ikikumbuka na mgogoro unaondelea wa Loliondo kati ya wazawa ambao ni wafugaji na wawekezaji lakini kama wananchi ndio wangekuwa wadau wakuu na wao wenyewe kuwa na nguvu ya kimaamuzi mgogoro usingelikuwepo.
Siamini na sidhani kama kuna mtanzania atakuwa akidhani na kuamini kuwa wawekezaji toka nje wanaweza tokea kuwa wadau wakubwa wa maendeleo kuliko wazawa tukiamini hivi tutalaaniwa na wazee wetu na tutalaumiwa na vizazi vijavyo ,mimi binafsi najenga imani yangu kuwa wazawa wenye asili hasa ya utanzania na anayejua kuwa asilimia 76.2% ya watanzania ni masikini na pato lao ni chini ya sh 1560.00/= sh za kitanzania kwa siku wakiandaliwa vizuri ,wakijengewa misingi mizuri ya uendesahwaji wa kisasi wa kukuza pato kubwa tunaweza siku moja kuwa kati ya taifa tajiri sana dunia.
Ahsanteni sana kwa kusoma napokea maoni yenu katika kuijenga Tanzania
Mungu wabariki Watanzania
My emails -: yuskamote@gmail.com
