thank you as a friend,relative and close friend to me because your reason to this success

thank you as a friend,relative and close friend to me because your reason to this success

Friday, April 11, 2014

ukomo wa ndoto na matarajio ya pan-africanists ,ni kiza kwa warithi wa leo wa fikra za pan-afrcanism

Tunaelekea wapi ????????????????????????

Maazimio ya Pan-Africanism yaliyowasilishwa na Kwame Nkrumah 1963 kama mwongozo wa waafrika kujikomboa,na kisha mapendezo endelevu juu ya mwongozo mkuu wa Nkrumah toka kwa Swaiba wake Julius Kambarage Nyerere 1966 na kuwasilishwa kwenye mkutano wa 1968 wa Pan-Africanism juu ya utamaduni wa kuheshimika kama mwafikrika na kuungana kuunda Taifa la Kiafrika tunayazika waasisi ambao kwetu tulikuwa taswira ya vipofu wasiyo juu tamu na radha ya kujitegemea chini ya nchi yenye mikataba toka Umoja wa Mataifa ,Leo Mtu mzima na akili timamu unasimama na kudai utegemezi wa kudhorotesha jitihada zile..ziko wap fikra za Pan-Africanism au tumesahaulishwa na marafiki waliojiita marafik wa maendeleo(wahisani) makosa yetu ni kuvaa koti la umasikini na kukosa upupu wa namna ya kulivua koti la ulowezi,unyonge na fikra mgando zilizoshawishiwa na adui wa Wazee wetu ,sishangai hata kujitafutia majibu ya maswali magumu kwa fikra nyepesi na kuamini kuna ukomo wa fikra za kutoka katika matatizo..,Lengo la kuanzishwa kwa Taifa la afrika ndio fikra tulifundishwa sisi na Kina Haroub Othman,Patrice Lumumbe Snr,JKN,Kwame Nkrumah ..Wazee wangu popote mlipo mimi mjukuu wenu Yusuph Kamote moyo wangu unabubunjikwa na machozi kwa kuona ndoto yenye mliyoniaminisha ipo siku nitaiona hata nami nifikiri uenda nikamrithisha mwanangu na Mwanangu akamrithisha mjukuu wangu ..,Tanzania kama sehemu ya kimfano kwa utekelezaji wa ndoto yetu Leo mliwafunza waturithishe wanatuambia nyie mlikosea na hamkujua kama wao wanavyojua ,Roho yangu imezizima kwa huzuni,misuli yangu imekosa nguvu ,Akili yangu ina maswali mengi yaliyo na Majibu ,Kizazi hiki kinafikiri kupata ufumbuzi kwa kuzika na kukwepa njia za kutatua matatizo ,Eti wanafikiri kutoka katika misuguano ya kimaslahi binafsi na wanafikiri maslahi ya Umoja huja kwa urahisi kama ilivyo maslahi ya mtu binafsi ,wanakimbia Msuguano wa kufika kwenye uimara wanafikiri katika ulegelege ..!mkiweza Wazee wangu huko mlipo nipewe ufumbuzi au mkishindwa basi nami ni mfu kama nyie kwa kuwa mawazo yangu hayaishi na Jamii hii ya leo..!MAJUTO YA MOYO NA ROHO YANGU yanatokwa na MACHOZI ndani ya mizunguko ya MISHIPA yangu ..!

Monday, February 10, 2014

NAVYOFIKIRI MIMI LEO HII

Leo katika wazo kuu hapa tunaangazia na kujaribu kufikirisha na kujifikirisha juu ya mkutano utakaofanyika alhamisi hii ya februari 13 2014 kule uingereza chini ya prince of wales,duke of cambridge ,David Cameroon and William Hague ,Rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania ,Mh Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kati yaya  viongozi 50 watakao wakilisha nchi zao katika mkutano huo ,huku kukiwa na majadiliano makali yakiendelea juu ya ripoti  ya ujangili wa tembo nchini Tanzania na ikikumbukwa kuwa agenda muhimu ya mkutano huu ni juu ya kufikia mikakati ya ulinzi wa viumbe hai na imadhamiriwa kutumika zaidi ya euro 5 billion kupambana na ukatili huo wa viumbe hai ,sio jambo jipya sana hapa kwetu kwani uliibuka mjadala uliopelekea kujiuzulu kwa baadhi ya mawaziri juu ya ripoti ya mapambano ya ujangili ikijulikana kama operesheni tokemeza ujangili ambayo utekelezaji wake ulikithiri katika vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kutajwa kwa watu wengi hasa viongozi waandamizi wa serikali na watu maarufu nchini na wakihusishwa kufanya biashara hii na wanaoitwa ni wafadhili na marafiki zetu katika maendeleo...Katika taarifa ya makala moja katika gazeti la MAIL la uingereza limejaribu kuhusisha hili na mahusiano yetu kimataifa hususani na bara la asia kama watekelezaji wa biasharra hii haramu na nchi baadhi za Afrika     (.http://www.dailymail.co.uk/news/article-2554773/Tanzania-slaughters-11-000-elephants-year-bloody-trade-tusks-President-turns-blind-eye-Prince-really-shake-hands-him.html)

1-tuzitafakari na kuzijadili kwa kujihadhari na hizi dalili nazoziita mvutano wa kimaslahi katika jumuiya ya kimataifa ,China na Tanzania ni marafiki wa kihistoria na hata kwa kipindi kirefu walikuwa wakiamini katika itikadi na kujenga mising ya kimaendeleo katika falsafa zilizokuwa zikifanana ,hofu yangu katika hili ni tunaweza kukubali kutumika katika kuaminishwa katika yale ambayo hayatakuwa sahihi sana ,hatutaweza kugharamikia gharama za chuki na fitna za watu ambao tunamfanano mzuri wa kihistoria na hata kiitikadi ,tunaitaji kuwa makini sana katika hili.

2-tuheshimu sana masslahi yetu kwa nguvu na mali ili kujilindia heshima yetu kitaifa na hata kimataifa kwa kuamini kuwa maslahi yetu hayatakuja kuaminishwa kuwa na mashirikiano na taifa lolote lile ila hatasita kuhusiana na yeyote yule atakayekuja kwetu kama rafiki na atakaye heshimu sera zetu za nje na atakaye heshimu maslahi yetu katika uhusiano huo.

3-Tatu na mwisho tuamini kuwa taifa letu ni changa na ni taifa huru mshikamano wa "kulinda maslahi na kutetea maslahi yetu utaongozwa kwa fikra zetu na maamuzi yetu kwa maridhiano yetu kwanza" na ushauri na maamuzi ya wengine yatafuata minyororo ile ile ya fikra zetu na maamuzi yetu kwa lengo kuu la kimsingi kuboresha na kamwe sio kuondoa maslahi yetu kwa kukithi tija na nia ya maslahi ya wengine kwa rasilimali zetu za ndani ya mipaka yetu.


Katika huru wa mwanadamu moja ya nyenzo kuu ninayoiamini ni uhuru wa fikra katika kutafakari na kutafakuri juu ya hoja..hivyovtuendelee kufikiri na kujadili juu ya hayo ili kujenga wazo kuu....

              ...........Asanteni kwa kuwa nami sasa tujadili tena katika wakati mwingine........

Sunday, February 9, 2014

umuhimu na tija ya kuhimizana kama vijana juu ya kusomana kuwekeza katika elimu lecture

                                                       PRESENTATION
                                        Comrade Yusuph KAMOTE
                      INSPIRATION FOR YOUTH STUDENTS PROGRAM
                                    GHOMME  SECONDARY  SCHOOL                             08/01/2014 
             
Awali ya yote napenda kutumia fursa hii hadhimu kumshukuru mwenyezi mungu ,muumba mbingu na ardhi kwa kutupa wasaha mzuri wa kunikutanisha mimi pamoja nanyi vijana wenzangu mchana huu.
Katika hali ya unyenyekevu mkubwa nimesimama mbele yenu si kama kiumbe mbora kuliko ninyi vijana wenzangu ila kama kijana mtiifu na mtumwa wa fikra za kuamini katika kukumbusha ,kuhamasisha na kujifunza kutoka kwenu juu ya masuala mbalimbali yenye athari chanya katika jamii zetu,hususani leo tunapozungumzia juu ya elimu na umuhimu wake kwa nafsi zetu na kwa taifa letu.
Elimu kwa mara kadhaa tumesikia ikiwa na kila maana ya tafsiri inayojaribu kutoa maana kuwa ni ujenzi wa kujikomboa ,kujiongoza na hata muhimili muhimu wa kupambana na changamoto mbalimbali katika jamii tunazoishi ,katika ujenzi wa taifa changa kama taifa letu Tanzania elimu ni msingi wa kutoa unyonge ,uonevu na ukandamizwaji wa minyororo ya umasikini wetu, hivyo kupitia siku hii nitawaomba kwa pamoja tutangaze vita ya kujikomboa,kujinasua na kujenga fikra pevu kupitia kusoma,kujifunza si kwa maana ya kuchukua fikra za kale kama silivyo na kuishi nazo leo hapana ila ni katika kujenga fikra mpya katika kukabiliana na changamoto za leo ili kuleta tija ya maendeleo na kasi ya maendeleo ya kidunia ,kama taifa tunaitaji sana wahandisi wengi,madaktari wengi katika fani tofauti tofauti ,tunaitaji wanasheria wengi ,tunaitaji wataalamu waliobobea wa masuala ya kitawala na kisiasa,tunaitaji sana sana wasomi wengi wa masuala ya utawala wa biashara na wahasibu na fani mbalimbali ,
SWALI LINAKUJA TUNAWAPATA VIPI NA WALIOJENGWA KWA FALSAFA ipi ya kielimu?
Katika kulijibu swali hili nitajielekeza katika sehemu mbinu kwanza kutoa moja ya dhaifu lililopo katika mfumo mzima wa elimu yetu na kutoa njia za kunasuka huko na kisha nitasema tutafika vipi huko ,naitaji usikivu wenu ulio tukuka hapa ;-
DHAIFU KUU-Moja ya dhaifu kubwa sana ninalofikiri mimi ni mfumo wa elimu yetu kukosa falsafa ya kuwajenga watu waamini katika nini na wanapaswa kuwa na majukumu gani  kwa taifa lao ambacho hiki kingelijenga tija ya wasomi wetu kujielekeza na kujiaminisha kuwa wao wanajukumu la kiukombozi katika taifa lao.
Madhara ya kuwa na mfumo usiojengeka katika falsafa yeyote ni watu kuamini katika yale yanayowaathiri katika jamii badala ya wao kuwa wahusika katika kutoa athari kwa msimamo wa kimfumo uliowalea(falsafa ya kielimu)
Mawazo yetu vijana wengi kuwa tunasoma ili kupata vyeo vikubwa(manager,officer,director,mbunge,waziri,rais) na kisha kuwa matajiri kwa kujihifadhia pesa nyingi kulikotokana na kusoma kwetu hii ni athari ya kijamii inavyoamini kwa mtu msomi, Ila mimi naomba kuiita hii ni athari ya Kukopa utamduni na kukosekana kwa falsafa ya elimu yetu kama taifa.
Kwa pamoja tuamini maisha ni hatua na hatua hizo huitajika sana mipango ,ufahamu na uelewa/weledi wa kupambana na changamoto zake na pesa,vyeo na mafanikio  ni matokeo ya vitu vinne ambavyo  leo nitavitumia kama jinsi gani tunaweza pata mafanikio katika kusoma kwetu na hata katika maisha yetu

JUHUDI/BIDII
Nafahamu kuwa msamiati huu katika mazingira haya ni msamiati wa kawaida sana ,ninaamini walimu na hata miongoni mwenu inawezekana kuwa na utamaduni wa kukumbushana juu ya kuongeza juhudi na bidii katika masomo yenu ,hivyo sitatumia mda mwingi sana hapa ,ila nachopenda kuwasihi vijana wenzangu juhudi pekee ndio siri ya mafanikio katika masomo yetu na hapa mahali popote pale panapoitaji ufanisi lazima juhudi iwepo ili tufikie mafanikio tunayojiwekea.

MAARIFA
Maarifa ni dhana pana ila ni kati ya yale tunayojifunza na kuyasoma kwa kujenga mazingira ya kujifunza zaidi ya yale walimu au mkufunzi anayotupa darasani kwani ,tunayapata vipi haya maarifa ni kupitia kupenda kusoma vitabu vya ziada juu ya mada tunazojifunza kwa lengo la kupanua zaidi uelewa wetu na kuyatumia hayo maarifa vyema zaidi katika mitihani na hatac maisha yetu na hapa ni vyema tujiwekee mazoea ya kupenda kusoma vitabu sana
.
MAADILI NA NIDHAMU
Kwa upande wangu ninaamini hiki ni kiini cha mafanikio masomoni na hata maishani ,kwani kwanza kitakujengea heshima na upendo kwa walimu na hata kwa jamii inayokuzunguka na watu watapenda kushirikiana nawe katika shughuli zako za kimasomo(discussion group),nina imani hapa shuleni kuna idara maalum na mwalimu wa nidhamu ambae kwenu kwa wachache wenu umuona kama adui ,mnoko wao lakini nataka kuwa shuhuda wenu leo huyu ni kiumbe bora kwenu kwani anasimama katika mafanikio yenu ya baadae,anawezaje na unaweza kumtumia vipi huyu?nina amini shule na hata nyinyi wenyewe mna timetable zenu ,moja za sifa za wengi waliofanikiwa ni wanaoheshimu na wenye nidhamu juu ya muda wao na mipango yao,nanyi mtakuwa kati ya waliofanikiwa kama mtaheshimu muda na mtakuwa na nidhamu juu ya utumijai wa muda wenu nyakati hizi za masomo yenu.

USHIRIKIANO NA WIVU WA KUFIKIA MALENGO

Nakumbuka kwa ukaribu mkubwa mara Zote nimekuwa nikiamini kuwa “kila binadamu mbele yangu ni faida na nimesogezewa kwa lengo moja tu kufaidika kwa uwepo wake” hii ikiwa na nana kuwa binadamu sisi tumebeba mema na mabaya katika tabia na mienendo yetu ,jukumu letu ni kujifunza vyote ili kuweza kujinasua na kuyaepuka yale mabaya yatakayo athiri malengo yetu na kushikamana na yale mazuri yatakayo boresha ukaribu wa kufikia mafanikio yetu  ,hivyo basi kujengea ushirikiano wa kila mmoja wetu katika masomo itatuwezesha kwa pamoja kufikia malengo katika masom yetu.
Kingine kama ziada ambacho ni cha msingi mno ni kuwashughulisha walimu kama sehemu ya kuwatumia katika kufikia malengo yako ya kujizidishia maarifa zaidi na kuhakikisha unamtumia yeye kama chombo chako cha kufikia ufaulu mzuri .
Kwa ujumla ukijiwekea misingi hii yote kama sehemu yako katika masomo na hata kimaisha jua utazalisha kile kinachokiita mafanikio katika maisha yake ni hizo pesa zitakuwa matokeo ya misingi ya hivyo vyote nilivyokwsisha waeleza vijana wenzangu.
Kwa kumalizia niwasihi tena na tena kuzingatia niliyowaeleza na watoa hoja wenzangu katika mhadhara huu waliyokwisha na watakayowaeleza .
Kwa mara nyingine tena niwashukuru sana tena sana Africa Youths Leadership Mark (AYLM TANZANIA) kwa mawazo na nia yao ya kudhubutu kuwafikia vijana na kuongea nao katika yale yenye tija na maslahi kwa taifa letu na pia niwashukuru kwa mualiko wao wa kunialika nije nitoe lecture hii kwenu kama kijana mwenzenu  ,nawashukuru sana.
         Mwenyezi mungu awape wepesi katika masomo yenu na awajalie nyie pamoja na taifa letu katika vita hii niliyoitangaza leo ya kujikomboa kupitia elimu ,sasa tupo mapambanoni na tusichoke kupigana paka mwisho .

                                                  ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA

Sunday, December 8, 2013

MAONI NA MCHANGO WANGU BINAFSI JUU YA MDAHALO/MJADALA WA UMILIKAJI WA RASILIMALI ZETU ,main agenda ikiwa ni GAS na rasilimali nyingine

Awali ya  yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema, vilevile niwapongeze UDASA kwa uendelezwaji midahalo na mada mbalimbali pamoja na kuwaalika viongozi waandamizi wa wizara hasa Mawaziri wahusika juu  ya hoja zinazoelekezwa katika idara wanazoziongoza kisiasa kwa maana kisera na kiusimamizi wa vipaumbele kwa niaba ya watanzania name pia kwa dhamira ya kupata majawabu juu ya sintofahamu zetu kitendaji , ikumbukwe mwezi August mwaka huu 2013 katika kongamano la Amani tulishuhudia mdahalo mzuri juu ya amani ya nchi yetu ,hivyo kwetu ilikuwa sehemu ya ushawishi  kufanya tafiti na kufatilia kwa ukaribu zaidi juu ya hoja mbalimbali zilizozungumziwa pamoja na Waziri mwandamizi wa Wizara ya mambo ya ndani ,Dr Emmanuel Nchimbi kutoa ufafanuzi.
Leo trh 08 Mwezi disemba ilikuwa  kuhusu Rasilimali zilizopo nchini na nafasi ya Mtanzania juu ya Rasilimali za nchini kwake....... .

Kimsingi kwa nadharia na mtazamo wangu, mimi naamin pamoja na mambo mengine yaliyozungumziwa nijikite katika mambo makuu mawili nayo ni yafuatayo -:
                                                                                    -KUAMINIANA na 
                                                     -USHILIKISHWAJI WA MWANANCHI NA RASILIMALI ZAKE

KUAMINIANA
Hii ni dhana ya msingi katika jamii yenye malengo na mikakati katika maswala yanayowahusu .
 kupitia matukio na majibizano ya wanasiasa na watanzania inaonekana hali ya watu kushawishiwa nje ya misingi ya kujenga ama kujenga hofu na kutomuamini mwingine imekuwa ni ndogo sana.
Nitoe mfano mmoja katika kuonesha faida zinazopatikana hasa kwa kiongozi kujenga imani ya kuwaamini anaowaongoza ambao kimsingi ndio wamiliki wa kwanza wa ardhi na wadau wakuu wa maendeleo kwani yanawahusu moja kwa moja wao..Moja ya matajiri wakubwa katika bara la Afrika ni Dangote lakini niliwahi kupata kusikia historia yake ya kutoka kuwa cement importer to  cement processing and manufacturing na imemjengea uwezo mkubwa kiuchumi na hasa kuchangia 3.5 billion USD kwa pato la mwaka katika nchi yake ,lakini haikuwa rahisi kwa dangote kupata mafanikio hayo peke yake ila iliwezekana kwa ushauri na kuaminiwa kwake na moja ya viongozi na serikali yake ndio imekuwa sababu ya utajiri wake ambao ni nuru kwa maisha ya Wanigeria leo hii.
Pamoja na ukweli kuwa uwezo wetu katika uchimbaji, umilikaji na uzalishaji wa nishati mbalimbali ikiwamo gesi ni mdogo na uenda ikawa ni vigumu kwetu lakini haiondoi ukweli kuwa bado mali hii ni ya Watanzania na hivyo wanastaili kufaidika moja kwa moja kupitia rasilimali zao na hata ikiwezekana wao kuwezesha na kuaminiwa kama walivyotengenezwa kina Dangote .
Naamini kwa Mwingi wa Rasilimali zetu na ustawi wa sekta binafsi na ukuaji wa pato la baadhi ya Watanzania bado serikali ina kila sababu ya kutengeneza kina Dangote 10 kwa wao kuchangia kiasi fulani katika mzunguko wa uchumi ubaki nchini na hivyo kujijengea uchumi imara na utakao kuwa kimbilio letu na si kuwa tegemezi tena katika bajeti zetu.

Katika hoja ya ushilikishwaji naomba niishauri serikali na Watanzania wenzangu kuwa "serikali na wadau wa maendeleo kuelekeza kupitia sheria mama/rasimu ya katiba mpya isomeke kuwa waratibu wakuu na mwenye maamuzi ya mwisho juu ya nani amiliki rasilimali fulani ndani ya maeneo ya wazawa wawe wanakijiji mwenyewe" kupitia maamuzi ya pamoja katika muundo wa  "mkutano mkuu wa kijiji "kwani ushilikishwaji wao kwa sasa unaonesha madhaifu makubwa ,kwa ukweli kuwa umekuwa wa kinadharia sana kuliko uhalisia hivyo :
                   Tubadili dhana  kuwa vyombo vya dola au halmashauri kuwa waamuzi wa mwisho bali wabaki kuwa wasimamizi na watekelezaji sera katika maeneo husika ila wasemaji wa mwisho juu ya rasilimali zao wawe wazawa/wanakijiji/wananchi hii itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi ikichochewa kwa kiasi kikubwa na Rasilimali zilizopo katika ardhi husika ikikumbuka na mgogoro unaondelea wa Loliondo kati ya wazawa ambao ni wafugaji na wawekezaji lakini kama wananchi ndio wangekuwa wadau wakuu na wao wenyewe kuwa na nguvu ya kimaamuzi mgogoro usingelikuwepo.

Siamini na sidhani kama kuna mtanzania atakuwa akidhani na kuamini kuwa wawekezaji toka nje wanaweza tokea kuwa wadau wakubwa wa maendeleo kuliko wazawa tukiamini hivi tutalaaniwa na wazee wetu na tutalaumiwa na vizazi vijavyo ,mimi binafsi najenga imani yangu kuwa wazawa wenye asili hasa ya utanzania na anayejua kuwa asilimia 76.2% ya watanzania ni masikini na pato lao ni chini ya sh 1560.00/= sh za kitanzania kwa siku wakiandaliwa vizuri ,wakijengewa misingi mizuri ya uendesahwaji wa kisasi wa kukuza pato kubwa tunaweza siku moja kuwa kati ya taifa tajiri sana dunia.

                        Ahsanteni sana kwa kusoma napokea maoni yenu katika kuijenga Tanzania
                                                              Mungu wabariki Watanzania
My emails -: yuskamote@gmail.com
                         Yusuphkamote@gmail.com

Saturday, December 7, 2013

HEKIMA NA BUSARA ZAKE KAMWE ZITAISHI TATA MADIBA

ilikuwa usiku wa Alhamisi trh ya 05 disemba 2013 ,nilipopokea taarifa kupitia televisheni ya BBC BREAKING NEWS ; Kuwa Mwenzetu ,Babu yetu ,Baba yetu na Mwanaharakati wa mapigano ya uhuru wa bara la Afrika na mtu aliyeamini na ameishi akimini kuwa haki ,usawa kwa wanadamu na uhuru kwa watu wote bila kujali rangi zao,tofauti zao za kiuchumi ,kisiasa na kijamii ni mambo si ya kunyang'anywa kama ilivyowahi kutokea South Africa 1940's paka 1994 ..kuwa AMEFARIKI DUNIA.
Ulikuwa usiku wa maajabu kwani kwa dakika na masaa kadhaa dunia nzima iliongea lugha na kauli moja juu ya kifo cha kipenzi cha watetea haki na watu wa itikadi zote.
Binafsi nimeanza kumfahamu Nelson Rolinhahla Mandela 1990's alipotembelea jijini Dar Es Salaam ,nikiwa bado na umri mdogo tulipata fursa za kwenda Airport kwa shamrashamra zote tukiimba nyimbo mbalimbali ,tyangu siku hiyo nilikuwa nikimsumbua baba aniadithie anavyomfahamu Tata Madiba ,alinitolea kitabu kidogo kilichoandikwa Madiba kilichotungwa 1994 ...sifa na mengi yaliyotukuka toka kwake ni ishara ya ushawishi wa Maadili mema na kuamini katika utawala bora.
siku zote tutaishi nawe katika fikra na mawazo yako yaliyotukuka ingawa hutokuwa nasi tena hakika wewe ni nembo na alama ya kuheshimika kwa bara letu na kila siku utakumbukwa...PUMZIKA SALAMA BABU TATA MADIBA..HAMBA KAHLE MADIBA

Monday, August 19, 2013

FIKRA KATIKA UTATUZI WA AJIRA NCHI ZA KIAFRIKA

Katika utafiti tuliopata kuufanya mapema mwaka huu kwa kutumia nchi za Tanzania ,Zimbabwe na Malawi utafiti unaonesha tatizo la ajira linazidi komaa zaidi kutokana na sera za kidunia za uhuru wa soko pamoja na fikra za upanuzi wa ajira kwa uwekezaji mkubwa wa sekta binafsi ,hali inayopelekea kuwa na wasomi wengi mitaani wanaokosa uwezo kimaandalizi juu ya kujitegemea kuliko kusubili kuajiliwa kutoka serikali au sekta binafsi ,Kwa tanzania peke yake inakadiliwa mwaka 2010 zilitolewa ajira 9000 kwa waombaji 24502 ambao wanasifa za shahada za kwanza na pili kitu ambazo ni tishio kubwa kuzaliwa wasomi ambao hawazalishi pato kubwa kwa serikali  yao tofauti na nchi kama Indonesia na Vietnam ambazo vijana wengi ndio chachu kubwa ya maendeleo ya nchi na ukuaji wa uchumi mkubwa ,ZINAFUATAZO ZINAWEZA ZIKAWA VYANZO VYA KUKOMOA TATIZO HILI KWA NCHI ZETU ;

1-Kuanzishwa kwa chombo maalumu cha kusimamia ukuaji wa ajira kwa vijana kupitia mfumo wa kujiajiri wenyewe kwa kuzingatia kuwa mfumo wa utoaji mkopo umeshindwa kuwa chachu ya madaliko ya haraka ya ukuaji uchumi kwa taifa kwani katika tafiti imeonesha wazi kuwa sera ya uwezeshwaji kwa makundi mbalimbali ilianzishwa tangu miaka 1980 na tangu kipindi hicho mafanikio yake yamekuwa yakulegalega hii inatokana na wawezeshwaji wengi wanashindwa kutekeleza mipango yao kwa kushindwa kuwa na utawala bora wa fedha hivyo ningelipenda kushauri kama ifuatavyo :
   
      a-kutotoa fedha taslimu kama mkopo na badala yake kutoa pembejeo au vifaa vya shughuli maalum ya muweshwaji.
      b-kuwa na chombo cha usimamizi wa uwekezaji katika kila wilaya kupitia sekta ndogo ndogo ambazo zitasaidia uombaji mikopo na utekelezwaji wa ombi la muhusika kwa msaada wa kitaaluma ili kumuwezeshaji afanikiwe katika shughuli zake

2-kuongeshwa kwa tafsiri za kisheria kama Enforcement Law ambazo zitakuwa na nguvu mpya na kubwa juu ya wawekazaji kuakikiza zalisho la ajira linakuwa kama lengo mojawapo la sekta binafsi kufanikiwa ipasavyo